Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei katika ujumbe wake ametoa rambirambi kwa kufuatia kuaga dunia Marjaa mtukufu, Hdhrat Ayatullah Haj Sheikh Ishaq Fayyadh. Aidha, amesifu huduma zake za kielimu za hawza na za uongozaji wa kidini, na kuwasilisha pole kwa Hawza ya Najaf Ashraf, wafuasi na wapenzi wa marehemu huyo, taifa la Afghanistan pamoja na familia yake.
Matini ya ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
إنا لله وإنا إليه راجعون
Habari ya kufariki Marjii mtukufu, Ayatullah Haj Sheikh Ishaq Fayyadh (Mwenyezi Mungu autakase udongo wake), imenitia huzuni na masikitiko makubwa, na imeiweka hawza hususan Hawza Tukufu ya Najaf Ashraf, katika maombolezo.
Miaka mingi ya uwepo wake katika Hawza Tukufu ya Najaf Ashraf na kunufaika na masomo ya wakubwa wake, kama marehemu Ayatullah Sayyid Abul-Qasim al-Khoei (r.a.), pamoja na kulea wanafunzi, kuandika vitabu, kusimamia mwenendo wa kielimu wa hawza hiyo, na kuwaongoza Waumini na wafuasi wa taqlidi, ni sehemu tu ya huduma za faqihi huyu ambazo hazitasahaulika, na athari zake njema zitaendelea kubaki, Inshaallah.
Mimi ninatoa pole kwa msiba huu mchungu kwa Hawza ya Najaf Ashraf, wafuasi na wapenzi wa Marjii huyo, hususan kwa taifa madhubuti na lisiloyumba la Afghanistan, pamoja na familia yake tukufu. Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe marehemu huyo mwema daraja ya juu na afufuliwe pamoja na mawalii wa Mwenyezi Mungu, na kwa waliobaki awape subira njema na malipo makubwa.
Sayyid Mujtaba Hosseini Khamenei
21 Khordad 1405 H.Sh. (11 June 2026).
Maoni yako